1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Matumaini ya maendeleo

3 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7a

Marais watatu wa Afrika wamesema kwamba bara lao sasa lina mawezekano makubwa ya kusonga mbele katika maendeleo kutokana na kuwekewa kipaumbele na nchi tajiri duniani.

Kauli hiyo imetolewa na marais Olusegun Obasanjo waNigeria,bwana Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda.

Viongozi hao wamesema kwenye mkutano wa nchi 19 za soko la pamoja, mashariki na kusini mwa Afrika COMESA mjini Kigali

kwamba bara la Afrika linaweza kusonga mbele ikiwa litatua migogoro inayozuia maendeleo.

Wajumbe kwenye mutano huo wa Kigali wamejadili mikakati itakayowezesha kuundwa kwa umoja wa forodha katika nchi za mashariki na kusini mwa Afrika hadi kufikia mwaka wa 2008.

Akizungumza kwenye mutano huo rais Paul Kagame Rwanda amesema kwamba nchi za Afrika haziwezi kunufaika na biashara ya kimataifa ikiwa kama migogoro na hali ya wasi wasi inafukuza vitega uchumi kutoka nje.

.