1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump adai kulengwa katika uchunguzi wa uchaguzi wa 2020

19 Julai 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema amepokea barua kutoka kwa wakili Jack Smith inayosema atachunguzwa na jopo la majaji, kuhusiana na juhudi zake za kutaka kupindua matokeo ya uchaguzi wa rais mwaka 2020.

https://p.dw.com/p/4U6b9
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwasili kuongea katika Klabu ya Gofu ya Taifa ya Trump Bedminster
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: John Angelillo/UPI Photo/IMAGO

Trump ameyasema hayo kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wake binafsi wa kijamii wa Truth Social. Mawakili wa Trump lakini hawakupatikana kwa ajili ya kutoa tamko kuhusiana na suala hilo, halikadhalika msemaji katika afisi ya wakili Smith, aliyepewa jukumu la kuyachunguza madai ya Trump.

Trump huenda akafunguliwa mashtaka ya jinai 

Barua hiyo ni ishara ya wazi kwamba Trump ambaye yuko mstari wa mbele katika kinyang'anyiro cha kuwania urais mwakani kupitia tiketi ya chama cha Republican, huenda akafunguliwa mashtaka ya jinai kuhusiana na juhudi zake za kutaka kusalia madarakani, hata baada ya kushindwa katika uchaguzi na rais wa sasa Joe Biden.