1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamerhe aunda muungano mpya wa kisiasa

24 Januari 2024

Mwanasiasa wa siku nyingi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vital Kamerhe, ameunda muungano mpya wa kisiasa unaoitwa PCR.

https://p.dw.com/p/4bdiZ
Rais Felix Tshisekedi wakati akiapishwa kwa muhula wa pili jijini Kinshasa.
Rais Felix Tshisekedi wakati akiapishwa kwa muhula wa pili jijini Kinshasa.Picha: Arsene Mpiana/AFP

Muungano huo mpya umeundwa ndani ya ule wa Union Sacrée unaovijumuisha vyama washirika wa Rais Felix Tshisekedi.

Kuundwa kwa PCR kumeibua wasiwasi  wa uwezekano wa kuyumba mshikamano miongoni mwa vyama vinavyoshirikiana na Rais Tshisekedi katika kuiongoza Kongo.  

Makundi manne ya kisiasa yanayounda muungano huo yanawajumuisha mawaziri wa uchumi Vital Kamerhe, Julien Paluku wa Viwanda na Jean-Lucien Bussa wa Biashara pamoja na kiongozi wa kundi la kisiasa la AAAP, Tony Kanku.

Kamerhe amesema muungano huo mpya utaimarisha mshikamano ndani ya muungano wa vyama tawala.  

Upande wa chama cha UDPS chake Rais Tshisekedi umesema hawajaona hasara au shida yoyote kuhusu kuwepo muungano huo ambao wanatumai umeundwa kwa maslahi ya taifa.