1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroBelarus

Je, Prigozhin atakuwa salama nchini Belarus?

28 Juni 2023

Makubaliano ya kumhamishia Prigozhin nchini Belarus yanamweka kiongozi huyo wa kundi la mamluki la Wagner chini ya taifa la ukandamizaji mkubwa. Je, nini kitatokea kwake?

https://p.dw.com/p/4TAsK
Ukraine | Krieg | Videostill Wagner-Chef Jewgeni Prigoschin
Kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin.Picha: Konkord Company Press Service/ITAR-TASS/IMAGO

Kiongozi wa mamluki wa Urusi Yevgeny Prigozhin alikuwa mkorofi kwa muda mrefu kwa utawala wa Putin hata kabla ya jaribio la uasi. Taarifa juu ya makubaliano ya kuhamia Belarus inamweka katika nchi ambapo tabia kama hiyo ni mwiko kabisa.

Siku ya Jumapili, Prigozhin alikuwa kimya kinyume na tabia yake wakati vikosi vyake vilipoondoka kwenye miji baada ya tangazo la serikali kwamba Prigozhin ameenda uhamishoni nchini Belarus.

Nini kitatokea kwa Prigozhin nchini Belarus?

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko aliripotiwa kufanya mazungumzo juu ya mpango huo na msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov ameeleza kuwa rais Lukashenko anaelewana na Mheshimiwa Prigozhin kwa muda mrefu muda wa miaka 20.

Lakini njia za Prigozhin zinapingana na njia za Lukashenko za kupambana na wapinzani na vyombo vya habari.

Soma pia: Yevgeny Prigozhin aeleza sababu za kufanya uasi

Ukandamizaji mkali wa Lukashenko wa vyombo vya habari vya upinzani na huru. Akiwa madarakani tangu 1994, kiongozi huyo anayeitwa dikteta wa mwisho wa  barani Ulaya alianzisha msako mkali dhidi ya maandamano ya mwaka 2020 yaliyofanwya kupinga utawala wake.

Mamia ya waandamanaji walihukumiwa vifungo virefu, ikiwa pamoja na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Ales Bialiatski.

Lukashenko ana usuhuba wa karibu na Putin

Alexander Lukashenko
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko.Picha: Mikhail Klimentyev/Kremlin/Sputnik/REUTERS

Chini ya Lukashenko, Belarus imekuwa kibaraka ya Urusi. Ingawa jeshi la Belarus halishiriki katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, Lukashenko ameiruhusu Urusi kuweka wanajeshi ambao walipigana nchini Ukraine. Urusi pia imepeleka silaha za nyuklia nchini Belarus. Lukashenko ni mshirika thabiti wa Rais Vladimir Putin.

Msimamo wa Prigozhin juu ya Rais Putin ni wa kiza kiza hata wakati wapiganaji wake walipokuwa wanaelekea Moscow siku ya Jumamosi.

Prigozhin hakufanya hivyo kwa sababu ya kumkosoa Putin moja kwa moja. Badala yake amesema lengo lake lilikuwa kuwaondoa madarakani viongozi wa majeshi ya Urusi ambao amewashutumu kwa ufisadi na uzembe.

Prigozhin amelalamika kwamba majeshi yake yaliathirika yalipokuwa yanapigana nchini Ukraine.

Soma pia: Urusi yasema Prigozhin hatashitakiwa

Kiongozi wa upinzani wa Belarus, Svetlana Tsikhanouskaya, aliyekimbia nchini amesema Lukashenko na Progozhin ni watu wasiokuwa na maelewano baina yao. Tsikhanouskaya amesema Lukashenko ameiweka nchi yake rehani. Ameiweka katika migogoro ya vita vya nchi nyingine.

Je, ni kwa muda gani Prigozhin atakaa nchini Belarus? Wachambuzi wanasema kiongozi huyo wa Mamluki amevuliwa madaraka yake juu ya vikosi vyake.

Wapiganaji wake wanaweza kujiunga na jeshi rasmi la Urusi au wanaweza kwenda Belarus. Taasisi ya wataalamu wa masuala ya kijeshi imeeleza hayo.

Je nini kinaweza kutokea endapo mamluki hao watakwenda Belarus ambako Urusi imeweka silaha zake za nyuklia za masafa mafupi? Naibu mkuu wa baraza la usalama la Urusi, Dmitry Medvedev amesema ana wasiwasi endapo mamluki hao watazifikia silaha hizo za nyuklia za Urusi.

Ametahadharisha kwamba dunia itatumbukia kwenye maafa ikiwa mamluki wa kundi la Wagner wataweza kuzidhibiti silaha hizo za nyuklia.