1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Janga la moto lauwa watu zaidi ya 70 Afrika Kusini

31 Agosti 2023

Moto uliozuka katika jengo la ghrofa tano katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini limesababisha vifo vya zaidi ya watu 70 huku wengine wengi wakijeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4VnW9
Südafrika | Großbrand in Johannesburg
Picha: Shiraaz Mohamed/REUTERS

Moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la jiji hilo kubwa la Johannesburg.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha jiji la Johannesburg, Robert Mulaudzi, moto huo umesababishapia watu wengine takriban 52 kujeruhiwa.

Soma pia:Watu wa 8 wamekufa kwa ajali ya moto.

Hata hivyo Mulaudzi amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi kwa kuwa jitihada ya kutafuta miili ya watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine inaendelea.

Katika taarifa yake ya ziada aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, kampuni ya awali iliyokuwa ikijulikana kama Twitter, msemaji huyo amesema watu kadhaa wameokolewa.

Jengo lililozuka moto ni makazi holela ya watu.

Pamoja na hiyo, akinukuliwa na vyombo tofauti vya habari nchini Afrika Kusini msemaji huyo amesikika akisema jengo hilo lililowaka moto lilikuwa linafanywa makazi kwa wasio na majumba.

Lakini pia mbali ya vifo vilivyotokana na moto, vipo vya baadhi ya watu ambao wanatajwa kufanya jaribio la kuruka kutoka katika jengo hilo refu,katika nyakati za usiku, kipindi ambacho moto huo unaendelea kwa lengo la kutaka kunusuru uhai wao.

Südafrika | Großbrand in Johannesburg
Jengo liliungua moto likiwa na idadi kubwa ya watu ndani mjini JohannesburgPicha: Michele Spatari/AFP/Getty Images

Msemaji Mulaudzi amenukuliwa akisema wanaendelea na shughuli ya uokoaji katika jengo hilo.

 "Mara tu tunapomaliza, tunakabidhi eneo la tukio, kwa polisi  kuendelea na kazi yao." Alisema Mulaudz

Jiji la Johannesburg na tatizo la uwepo wa majengo holela ya zamani.

Eneo hilo la kati la Johannesburg limekuwa na majengo yaliyotelekezwa au kuanza kuvunjika na mara nyingi yanatumiwa kama makazi na watu wenye shida ya malazi.

Mamlaka ya jiji huyataja aina hiyo ya majengo kama "majengo yaliyotekwa nyara." Duru zinaeleza jengo hilo lilikuwa wakazi ya takribani watu 200.

Soma pia:Watu 15 wafariki kwenye ajali ya moto kiwandani, Ufilipino

Shuhuda mmoja ambae anaishi karibu na jengo hilo alikiambia kituo kimoja cha televisheni nchini Afrika Kusini kuwa wakati moto ulipoanza alisikia sauti ya vilio vya watu vya kuomba msaada, wakisema "wanakufa".

Soma zaidi:SADC: Uchaguzi Zimbabwe haujakidhi mahitaji ya katiba

Hadi wakati huu chanzo rasmi cha moto huo, bado hakijajulikana na maafisa wanaendelea na uchunguzi wao.

Lakini Afisa mmoja wa serikali za mitaa katika eneo hilo, Mgcini Tshwaku amesema inaonekana kama kuna mkazi mmoja aliwasha motokwa lengo la kupasha joto makazi kwa ajili ya kujikinga na hali ya baridi.

Moto wateketeza mali soko la Karume kwa mara nyingine

 

,