1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

Watu 29 wafariki katika ajali ya moto kwenye hospitali China

19 Aprili 2023

Watu 29 wamekufa katika ajali ya moto iliyotokea kwenye hospitali ya Changfeng mjini Beijing, na kwa mujibu wa taarifa rasmi, watu 12 wamekamatwa kuhusiana na mkasa huo

https://p.dw.com/p/4QHba
China I Nach Brand im Changfeng Krankenhaus in Peking
Picha: Greg Baker/AFP

Naibu mkuu wa huduma za zima moto mjini Beijing amesema yumkini moto huo ulisababishwa na shughuli za ukarabati zilizokuwa zikifanyika katika hospitali hiyo. Miongoni mwa waliokamatwa ni mkuu wa hospitali ya Changfeng na maafisa wawili wa kampuni ya ujenzi iliyohusika.

Huduma za wazimamoto zimefanikiwa kuwaoka wagonjwa 142 kutoka kwenye jengo la hospitali hiyo lililokuwa likiwaka moto na kuwahamishia katika ituo vingine vya matibabu.

Ripoti za vyombo vya habari zimeeleza kuwa wengi wa waliouawa ni vikongwe waliokuwa wamelazwa hospitalini wakiwa hawana nguvu za kukimbia. Serikli imeamuru ukaguzi wa kiusalama katika hospitali zote baada ya ajali hiyo.