1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUfilipino

Watu 15 wafariki kwenye ajali ya moto kiwandani, Ufilipino

31 Agosti 2023

Moto uliozuka kwenye kiwanda kimoja kidogo cha kukata vitambaa vya kutengeneza bidhaa mbali mbali umeua watu 15 nchini Ufilipino asbuhi ya leo Alhamisi.

https://p.dw.com/p/4VnHQ
Philippinen Manila | Gebäude des Post office abgebrannt
Picha: BUREAU OF FIRE PROTECTION NCR/REUTERS

Wengi waliokufa kwenye moto huo ni wafanyakazi wa kiwanda hicho ambacho kiko katika eneo la makaazi ya watu.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa shirika la kuzuia moto, watoa huduma ya zima moto walichelewa kufika kutokana na mafuriko,msongamano wa magari na kukosea anuani ya kiliko kiwanda hicho.

soma pia:

Wengi waliokufa walikuwa wamelala kwenye vyumba vyao wakati moto ulipozuka na watu watatu walinusurika na kupelekwa hospitali kutokana na  majeraha walopata baada ya kuruka kutoka ghorofa ya pili.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW