1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Haiti uko Kenya kujadili juu ya kutumwa kwa askari

14 Desemba 2023

Ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Haiti uko nchini Kenya kutathmini maandalizi ya maafisa wa polisi wa Kenya ili kukabiliana na ghasia za magenge katika taifa hilo la Karibik.

https://p.dw.com/p/4a8xt
Haiti | Polisi wakirushiana risasi na magenge ya uhalifu
Polisi Haiti wakiwa katika oparesheni ya kuyaondoa magenge ya uhalifuPicha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Mkurugenzi mtendaji wa polisi wa taifa wa Haiti, Frantz Elbe, na ujumbe wake uliwasili Nairobi siku ya Jumanne kwa ziara ya siku tatu, kwa mujibu wa taarifa ya afisi ya Inspekta mkuu wa polisi,Japheth Koome.

Duru zinaeleza kuwa ujio huo ni baadhi ya maandalizi ya kikosi cha maafisa alfu moja wa Kenya kujiunga na wenza wao alfu tatu watakaoshika doria mjini Port-Au-Prince chini ya mwamvuli wa ujumbe wa pamoja wa kuimarisha usalama, MSS, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Soma pia:Kenya yasema haitopeleka askari Haiti hadi Umoja wa Mataifa utoe fedha

Maafisa wanasema kuwa Kenya itapeleka kikosi cha kwanza cha maafisa 300 wa polisi nchini Haiti ifikapo Februari kama sehemu ya Ujumbe wa Kimataifa wa Kusaidia Usalama unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Mahakama ya Kenyaitatoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga kutumwa mnamo 26 Januari 2024.

Ni kwa nini Kenya imejitokeza kupeleka polisi wake Haiti?