1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza:Israel yauwa katika kambi ya wakimbizi.

21 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5O

Huko kusini mwa Israel, jeshi la nchi hiyo wameshambulia huko Gaza katika kambi ya wakimbizi ya Maghazi baada ya siku mbili za hujuma.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, vikosi vya Israel vimewauwa watu kiasi ya 14 wengi wao wakiwa wanamgambo wa kiislamu wa ki-Palestina.

Israel imesema mwanamgambo mmoja aliyeuliwa alitaka kuripua roketi dhidi ya Israel.

Hujuma za Israel huko Gaza zilizoanza mwezi uliopita kwa ajili ya kumkomboa mwanajeshi wao aliyetekwa nyara, tayari zimesababisha wapalestina zaidi ya 110 kuuwawa.

Kundi moja la wanamgambo wa kipalestina lenye umaarufu nchini humo lijulikanalo kama Popular Resistance Committee limesema kuwa „Israel italipia thamani kubwa kwa hasara walizozisababisha“.