1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 inahitaji kuongeza wanachama

7 Septemba 2023

Mkuu wa Kongamano la Usalama la Munich, Christoph Heusgen amesema anaunga mkono kuongeza wanachama wa kundi la mataifa saba yaliyoendelea zaidi kiviwanda duniani, G7 ili kulifanya jukwaa hilo liendelee kuwa na umuhimu.

https://p.dw.com/p/4W3Tp
Deutschland | Münchner Sicherheitskonferenz | Christoph Heusgen
Picha: Thomas Kienzle/AFP/Getty Images

Heusgen ameliambia shirika la habari la DPA kuwa, moja ya sifa za kundi hilo ni ukweli kwamba linahusu mataifa yenye maadili yanayofanana. Ameongeza kuwa, nchi kama vile Korea ya Kusini na Australia zinaweza kujiunga ili kuliongezea nguvu kundi hilo.

Soma pia: NATO, G7 kuendelea kuibeba Ukraine

Mkuu huyo wa kongamano la usalama la Munich linalowakusanya pamoja viongozi wa mataifa na maafisa wa ngazi ya juu wa sera za ulinzi na masuala ya kigeni, amesema hata hivyo uzito wa mataifa hayo kiuchumi umepungua, hivyo kulitanua ni jambo lenye mantiki.

Mataifa yanayounda kundi hilo laG7 ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa, Italia, Japan, Canada, Marekani na Uingereza.