1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mataifa ya G7 yadhamiria kuiunga mkono Ukraine

21 Mei 2023

Viongozi wa mataifa tajiri duniani yanayounda kundi la G7 wameonesha umoja katika kuiunga mkono Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi katika mkutano wa kilele uliofanyika mjini Hiroshima.

https://p.dw.com/p/4RdIB
G7 Gipfel in Japan, Hiroshima | Narendra Modi und Wolodymyr Selenskyj
Picha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliyehudhuria  mkutano huo amejihakikishia kupatiwa silaha zaidi pamoja na uungwaji mkono wa kidiplomasia wakati wanajeshi wake katika uwanja wa mapambano kwenye mji wa Bakhmut wakikabiliwa na mkwamo.Waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida, amesema, kuhudhuria kwa Zelensky kwenye mkutano huo wa siku tatu uliofikia tamati leo, kumesaidia kutuma ujumbe mzito kwa dunia na kwamba lilikuwa jambo muhimu. Kishida ameongeza pia kuwa, kitisho cha matumizi ya silaha za nyuklia hakipaswi kukubalika popote pale duniani akizungumzia viashiria vya Urusi kutaka kufanya hivyo katika miezi iliyopita.