1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FC Cologne yatamba mbele ya B.Munich

23 Februari 2009

Hamburg yaongoza Bundesliga

https://p.dw.com/p/GzkV
Wachezaji wa FC Cologne wakishangiria.Picha: AP

FC Cologne, yazusha msangao katika Bundesliga baada ya kuwachezesha kindumbwe-ndumbwe mabingwa Bayern Munich na kuwazaba mabao 2-1-

na Katika la Liga-ligi ya Spain, mkosi ulioipata Bayern Munich kulazwa na chipukizi FC Cologne, umewapata viongozi wa Ligi FC Barcelona kwani ,wameteleza mbele ya timu inayoburura mkia Espanyol.

Tutawachukua pia Abidjan ,Ivory Coast ambako kinyanganyiro cha Kombe la Afrika la wachezaji wasiolipwa ,Taifa Stars-timu ya taifa ya Tanzania imeanza vibaya ilipotolewa jana kwa bao 1-0 na Senegal.

Mwaka mpya haukuanza uzuri kwa wababe 2 wa dimba la Ujerumani:Mabingwa Bayern Munich na Werder Bremen:

Mabingwa Bayern Munich ,walikiiona cha mtema kuni hapo jumamosi walipopata pigo lao la 3 mwaka huu mpya mara hii kutoka FC cologne.

Kwanza alikuwa mfaransa Fabrice Ehret alielifumania lango la Bayern munich kabla ya Daniel Brosinski,alieichezea FC Cologne kwa mara ya kwanza kuupiga msumari wapili katika jeneza la Bayern Munich-hivyo kuanuzisha rasmi shangwe na shamra shamra za kanivali mjini Cologne.

Jane Nyingi anatuchukua uwanjani:

Munich ilimleta uwanjani kwa mara ya kwanza tangu mwanzo mshambulizi wao Lukas Podolski,anaerudi FC Cologne, msimu ujao ili aifedhehi klabu yake hiyo ya nyumbani,lakini hata Podolski,hakufua dafu siku hiyo.

Kwani, kipindi cha pili alipumzishwa na kuitwa uwanjani muamerika Landon Donovan aliefaulu tu kuokoa bao la 3 la Cologne katika chaki ya lango lake.

Baada ya ushindi huo mkuu,kocha wa FC Cologne Christopher Daum,ambae hakuishinda Munich tangu kupita miaka 17 alikuwa na haya kusema:

"Kuweza kushinda nyumbani mwa timu nionavyo mimi ni mabingwa wajao,ni jambo la maana sana.Hata ikiwa ni baada ya kitambo kirefu,kuishinda Bayern Munich mjini Munich ni tokeo maalumu linalonivutia sana."

Alisema kocha wa FC Cologne ambayo sasa inakaribia kutimiza shabaha yake ya kubakia daraja ya kwanza msimu ujao.

WSerder Bremen ni mbabe mwengine wa bundesliga anaepepesuka ,kwani baada ya kumudu suluhu ya bao 1:1 nyumbani na AC Milan ya Itali katika kombe la ulaya la UEFA kati ya wiki,wengi walitarajia wangetamba mbele ya Energie Cottbus.

Lakini mwishoe, ilionesha Energie Cottbus ina nguvu zaidi kuliko Bremen.Ingawa jogoo lao mbrazil Diego lilibanwsa barabara na halikufurukuta, Hugo Almeida,alitangulia kuipatia Breme bao.Lakini Ivica Iliev na Dimitar Rangelov,waliiambia Bremen "kutangulia, si kufika".

Kwa mabao 2:1, vishindo vya darini vya wababe Bremen vikaishia sakafuni mjini Cottbus.

Baada ya chipuklizi Hoffenheim kumdu suluhu tu ya mabao 3:3 hapo ijumaa na Stuttgart,Hamburg jana ilivunja ubishi wa Bayer Leverkuseb mjini Dussldorf na kuondoka na pointi 3 ilizohitaji kuparamia kileleni mwa Bundesliga. Na sasa ni Hamburg inayoongoza baada ya Hertha berlin iliokua kileleni kabisa kutimuliwa kwa mabao 2-1 na Wolfsburg.

Huko Abidjan,Corte d-Iviore au Ivory Coast firimbi ililia mwishoni mwa wiki kuanzisha Kombe la Afrika la mataifa kwa wachezaji wasiolipwa.Tanzania inashiriki katika kombe hilo na hii ni wiki baada ya ufunguzi rasmi wa Uwanja mpya wa Taifa mjini Dar-es-salaam. Tanzania lakini ilianza vibaya kwani ililazwa bao 1:0 na Senegal.Wenyeji Ivory Coast walitandikwa mabao 3:0 na Zambia.Timu 8 zinashiriki pamoja na Ghana na simba wa nyika Kamerun.

Vipi ligi nyengine mashuhuri za ulaya zilipita mwishoni mwa wiki ?

Hadi wiki 2 nyuma, hakuna alietia shaka kwamba, taji la ubingwa la La Liga-

Ligi ya Spian,msimu huu linaenda Barcelona.Klabu hiyo ya mkamerun Samuel Eto-o anaeongoza katika watiaji magoli,ikiongoza kwa pointi 12 mbele ya mahasimu wao wa jadi -mabingwa Real Madrid.Aklina Eto-o na muargentina Lionel Mess, wamekuwa wakitamba a