1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droni za Urusi zaushambulia mji wa Odesa kwa saa tatu

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2023

Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika maeneo ya kusini mwa Odesa mapema leo. Kyivv imesema, mashambulizi hayo yaliyofanywa kwa muda wa saa tatu na nusu yameipiga miundombinu ya bandari ya mto Danube.

https://p.dw.com/p/4Vte7
Odessa
Moja ya jengo lililoharibiwa katika mashambulizi ya Urusi huko OdesaPicha: Andre Alves/AA/picture alliance

Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika maeneo ya kusini mwa Odesa mapema leo. Kyivv imesema, mashambulizi hayo yaliyofanywa kwa muda wa saa tatu na nusu yameipiga miundombinu ya bandari ya mto Danubena yamewajeruhi watu wawili.

Jeshi la anga la Ukraine kupitia mtandao wa Telegram limeandika kuwa mifumo yake ya ulinzi wa anga ilizidungua droni 22 kati ya 25 za Urusi zilizotengenezwa Iran ambazo zilielekezwa Odesa.

Mto Danube umekuwa njia kuu ya kusafirishia nafaka tangu mkataba wa usafirishaji wa bidhaa za kilimo kupitia Bahari nyeusi uliokuwa ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa ulipovunjika mwezi Julai.

Muda mfupi kabla ya mashambulizi hayo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kuwa meli mbili zaidi za mizigo zilifanikiwa kupita njia ya muda iliyoanzishwa na Kyiv katika eneo hilo.