1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miundombinu ya banadari ya Odesa yashambuliwa na Urusi

2 Agosti 2023

Urusi imefanya shambulio la ndege zisizokuwa na rubani aina ya Shahed zilizotengenezwa Iran na kulenga miundombinu ya bandari katika mkoa wa Odesa usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4Ugai
Ukraine | Drohnenangriff auf Odessa
Picha: Telegram/Oleh Kiper/AP/picture alliance

Jeshi la Ukraine limeripoti uharibifu wa ghala la nafaka na kusababisha moto katika vifaa vinavyotumika kusafirisha nafaka muhimu nchini humo.Kamandi ya jeshi la Ukraine upande wa kusini mwa nchi hiyo imeandika kwenye mtandao wa Facebook kuwa, lengo la adui ni kuvishambulia vifaa vya bandari na miundombinu muhimu katika mkoa huo.Tangu kujiondoa kwenye mpango wa usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi, Urusi imefanya mashambulizi ya mara kwa mara yanayoilenga bandari ya Odesa.