1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donald Trump atafanya mkutano wake wa kampeni huko Michigan

20 Julai 2024

Mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump Jumamosi anafanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni katika kinyang’anyiro hicho katika jiji la Michigan

https://p.dw.com/p/4iXIk
Donald trump
Mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump Jumamosi anafanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni katika kinyang’anyiro hicho katika jiji la MichiganPicha: Matt Rourke/AP Photo/picture alliance

Mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump Jumamosi anafanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni katika kinyang’anyiro hicho katika jiji la Michigan.

Maalfu ya wafuasi wake walikuwa tayari wamepanga mstari tangu jana Ijumaa jioni nje ya uwanja wa Van Andel Arena kila mmoja akiwa na hamu ya kupata nafasi za kwanza za kuruhusiwa kuingia uwanjani humo.

soma zaidi. Trump: Nagombea kuwa Rais wa Marekani yote

Trump ataingia kwenye uwanja huo na mgombea wake mwenza atayekuwa makamu wake J.D. Vance.

Kwa upande wa chama cha Democratic, Rais Joe Biden anakabiliana na uasi wa ndani ya chama chake kutoka kwa wabunge wakuu na wafadhili wanaomtaka rais huyo mwenye umri wa miaka 81 ajiondoe kwenye kinyang'anyiro hicho.