1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aapa kushinda pamoja na kushinikizwa ajiengue

20 Julai 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amesisitiza kuwa atasalia katika kinyang'anyiro cha uraisi, licha ya kupingwa na baadhi ya Wademocrats, na kuzua uvumi kwamba anaweza kujiuzulu katika siku hizi za mwisho wa juma.

https://p.dw.com/p/4iX2N
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais Joe Biden akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la 115 la NAACP huko Las Vegas, Julai 16, 2024. Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa yake kutoka katika makazi yake ya ufukweni huko Delaware anakojitenga baada ya kupata maambukizi ya UVIKO-19, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 amesema atarejea katika pirika za kampeni juma lijalo.

Katika mwendelezo huo wa kampeni anatarajiwa kujibu mapigo ya hotuba ya Donald Trump ambayo aliwasilisha katika mkutano wa chama chake cha Republican wa kuridhia kuwa mgombea wa chama hicho.

Lakini ukaidi wake unakuja katika kipindi ambacho viongozi wenginesita waandamizi wa chama chake kumtaka ajiuzulu katika uchaguzi wa Novemba kwa sababu ya wasiwasi wa kupoteza kura nyingi na mashaka juu ya afya yake.