1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DFB: Ubaguzi wa rangi bado ni tatizo soka la Ujerumani

12 Septemba 2023

Ubaguzi wa rangi katika soka la Ujerumani bado ni tatizo. Hayo ni kulingana na takwimu za ofisi ya usajili wa kesi za ubaguzi wa rangi katika jimbo la North Rhine-Westphalia.

https://p.dw.com/p/4WEyO
Wachezaji wa timu ya soka Ujerumani
Wachezaji wa timu ya soka UjerumaniPicha: Bahho Kara/Eibner/IMAGO

Ofisi hiyo imesajili matukio 211 yanayoweza kutafsiriwa kuwa ya kibaguzi, 95 kati ya matukio hayo yakitokea kwenye soka la kulipwa tangu Julai mwaka 2022.

Idadi hiyo ni kubwa kuliko takwimu zilizotolewa na shirikisho la soka la Ujerumani DFB ambalo limebainisha kesi tatu za ubaguzi wa rangi msimu uliopita.

Soma pia:Ujerumani kutoa msaada zaidi kwa Ukraine wakati ikiendelöeza harakati za jkuyakomboa maeneo yake yanayokaliwa na Urusi

Msemaji wa shirikisho hilo Michael Morsch amesema DFB iliorodhesha matukio 35 ya ubaguzi wa rangi katika msimu wa mwaka 2016-17 na kuelezea masikitiko yake juu ya ongezeko la visa vya ubaguzi.