1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaiahidi Ukraine msaada wa dola milioni 21

12 Septemba 2023

Ujerumani imeahidi kuipatia Ukraine msaada ziada wa kiutu wa kiasi dola milioni 21 lakini imjezuia kutoa msimamo wa wazi juu ya iwapo itapitia Ukraine makombora ya masafa marefu aina Taurus.

https://p.dw.com/p/4WCgj
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock(mwenye miwani myeusi) akisikiliza jambo wakati wa ziara yake mjini Kyiv Septemba 11, 2023.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock(mwenye miwani myeusi) akisikiliza jambo wakati wa ziara yake mjini Kyiv Septemba 11, 2023.Picha: Jörg Blank/dpa/picture alliance

Tangazo la msaada huo wa nyongeza limetolewa na waziri wa mambo ya kigeni wa UjerumaniAnnalena Baerbock aliye ziarani nchini Ukraine baada ya kukutana na mwenzake wa Ukraine, Dmytro Kuleba. 

Ama kuhusu suala la makombora ya Taurus, Baerbock amesema Ujerumani bado haijafikia uamuzi wa kutuma makombora hayo yenye uwezo mkubwa na asingeweza kutoa ahadi kabla ya mwafaka kupatikana, msimamo ambao yumkini haukumfurahisha waziri mwenzake wa Ukraine ambaye ameirai Ujerumani kutopoteza wakati:

"Tungekuwa tumepata mafanikio zaidi na kunusuru maisha ya wanajeshi wa Ukraine na raia kama tungekuwa tumepata makombora ya Taurus. Tunaiambia serikali ya Ujerumani kwamba tunaheshimu majadiliano yenu lakini kwa tunachofahamu hakuna msingi wowote hadi sasa wa kupinga kutupatia silaha hizo."

Ukraine inaamini makombora hayo ya Taurus yataiwezesha kuvikabili kwa uzani ulio sawa vikosi vya Urusi vilivyoivamia nchi hiyo Februari mwaka jana.