1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COP28 yazindua mfuko wa hasara na uharibifu wa tabianchi

30 Novemba 2023

Mkutano wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, COP28 umezindua siku ya Alhamisi, mfuko wa kufidia hasara na uharibifu utokanao na mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yalioko hatarini kuhusiana na ongezeko la joto duniani.

https://p.dw.com/p/4ZcrT
Dubai COP28
Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, pamoja na Ujerumani zimechangia dola milioni 100 kila mmoja kwenye mfuko wa fidia ya hasara za mabadiliko ya tabianchi.Picha: Rafiq Maqbool/AP/dpa/picuture alliance

"Tumewasilisha historia leo," rais wa UAE wa COP28,Sultan Al Jaber aliwaambia wajumbe, akiongeza kuwa nchi yake ilikuwa ikitoa dola milioni 100 kwa mfuko huo. Ujerumani pia imeahidi kutoa dola milioni 100.

Baada ya miaka mingi ya kujiburuza juu ya suala hilo, mataifa tajiri yaliunga mkono mfuko huo katika makubaliano ya kihistoria katika mkutano wa kilele wa COP27 mjini Sharm el-Sheikh nchini mwaka jana.

Soma pia: Rais wa mkutano wa mazingira wa COP28 akanusha ripoti kuwa UAE inataka kutafuta mikataba ya mafuta

Uzinduzi wake katika siku ya kwanza ya COP28 mjini Dubai unafuatia mazungumzo magumu kuhusu utaratibu wa mfuko huo, ambao utawekwa katika Benki ya Dunia kwa muda mfupi.

"Hii inatoa ishara chanya ya kasi kwa ulimwengu na kwa kazi yetu," Jaber alisema.

Jaber alisema "ni mara ya kwanza uamuzi kupitishwa siku ya kwanza ya COP yoyote na kasi ambayo tumefanya hivyo pia ni ya kipekee, ya ajabu na ya kihistoria."

"Huu ni ushahidi kwamba tunaweza kutoa. COP28 inaweza na itatoa," aliongeza.