1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa COP28 akanusha UAE haitafuti mikataba ya mafuta

29 Novemba 2023

Rais wa mkutano wa mazingira wa COP28 akanusha ripoti kuwa UAE inataka kutafuta mikataba ya mafuta.

https://p.dw.com/p/4Zauu
Mazingira | Raisbwa COP28 Sultan Ahmed Al Jaber
Rais wa Imarati kwa ajili ya mazungumzo yajayo ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa - COP28Picha: Sascha Schuermann/Getty Images

Rais mteule wa Imarati kwa ajili ya mazungumzo yajayo ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa - COP28 amekanusha vikali ripoti inayodai kuwa taifa lake lilipanga kutumia mkutano huo wa kilele ili kufikia mikataba ya mafuta na gesi, siku moja kabla ya mkutano huo kuanza.

Sultan al-Jaber, ambaye anasimamia kampuni kubwa ya mafuta ya Abu Dhabi National Oil inayoendeshwa na serikali, ameyaita madai hayo kutoka kwenye ripoti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC kuwa ni "jaribio la kuhujumu kaziya urais wa mkutano wa COP28" kabla ya kuanza mazungumzo hayo kesho Alhamisi.

Soma pia:Guterres atoa wito kuongeza juhudi kukabiliana na tabia nchi

Ripoti hiyo ilitaja kile ilichokielezea kuwa ni "nyaraka zilizovujishwa ambazo shirika hilo la utangazaji la Uingereza lilisema zilionyesha kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu ulipanga kujadili mikataba ya mafuta ya visukuku na mataifa 15.

Sultan Al Jaber amewaambia waandishi habari kuwa tuhuma hizo ni za uwongo na kwamba taifa hilo limekuwa wazi katika namna linavyotaka kuendesha mchakato huo waCOP28.