1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN: Wanawake wakumbuka maandamano ya kupinga ubaguzi

9 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDN7

Kwa maelfu,watu wameandamana kwa furaha hadi makao makuu ya serikali nchini Afrika Kusini, kukumbuka maandamano yaliyofanywa na wanawake miaka 50 ya nyuma,kupinga sera za ubaguzi za serikali ya hapo zamani.Lakini sherehe hizo zimetiwa doa na ukweli kuwa wanawake katika taifa jipya la Afrika ya Kusini lenye udemokrasia, wanawake ndio wameathirika vibaya zaidi na umasikini,janga la Ukimwi.Vile vile wanawake nchini humo wanakabiliwa na ukatili wa majumbani mwao na ubakaji,kuliko ko kote kwingine duniani. Rais Thabo Mbeki,hii leo alipowapokea waandamanaji alisema,wanawake wengi hawakupata matunda ya ukombozi.Akaongezea kuwa serikali yake itahimiza juhudi za kuendeleza haki za wanawake. Mwaka 1956,kiasi ya wanawake 20,000 waliandamana mbele ya makao makuu ya serikali kupinga sheria ya kuwataka wanawake kama vile wanaume wa Kiafrika kubeba vyeti vya utambulisho vilivyowazuia kuingia maeneo fulani.