1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Burundi yaishtumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi

30 Desemba 2023

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameishtumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wanaolaumiwa kwa kuhusika na mkururo wa mashambulizi kwenye ardhi ya nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4aih3
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi Evariste NdayishimiyePicha: Rafiq Maqbool/AP/picture alliance

Burundi imesema kundi la waasi la RED-Tabara lilifanya shambulio Desemba 22 karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kuuwa watu 20, wakiwemo wanawake na watoto.

Soma pia: Shambulizi la waasi lasababisha vifo vya watu 20 Burundi

Akizungumza katika mkutano uliotangazwa na vyombo vya habari vya Burundi kutokea mashariki mwa Burundi, Rais Ndayishimiye alisema makundi hayo ya waasi yamepewa hifadhi, chakula, ofisi na fedha kutoka nchi inayowakaribisha, na kuitaja Rwanda.

Ndayishimiye ameapa kupambana dhidi ya kundi hilo kwa nguvu zote. Hata hivyo kundi hilo na serikali ya Rwanda walikanusha madai hayo.