1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BURMA.Burma yakosolewa juu ya Aung San Suu Kyi

17 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF2f

Mjumbe wa masuala ya haki wa Umoja wa Mataifa amesema kitendo cha serikali ya Burma cha kuendelea kumuweka kwenye´kifungo cha ndani ya nyumba mwanademokrasia Aung San Suu Kyi ni cha kusikitisha mno.

Akizungumza kutoka Bangkok, Paulo Sergio Pinheiro amesema nchi hiyo inastahili kuharakisha mpango wa kufanya mageuzi.

Utawala wa kijeshi umekataa kumuachilia mshindi huyo wa tuzo ya amani Nobel au kumruhusu ajihusishe kwenye masuala ya siasa.

Suu Kyi amekaa ndani zaidi ya miaka miwili iliyopita baada ya kuvamiwa pamoja na wafuasi wake na wanaunga mkono utawala huo.

Matamshi ya mjumbe huyo yamekuja baada ya Waziri mkuu wa zamani wa Malysia Mahathir Mohamad kuwatolea wito magenerali wa utawala huo wa kijeshi kumuachilia huru kiongozi huyo anayetimiza miaka 60 tangu azaliwe hapo jumapili.