1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Wawili wahukumiwa miaka 12 jela kwa mauaji ya Rwanda

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEyy

Mahakama ya Ubelgiji imewahukumu kifungo cha hadi miaka 12 jela wafanyibiashara wawili wakiruanda kwa makosa ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Wazee wa mahakama hiyo waliwapata na hatia Etienne Nzabonimana na kakake wa kambo Samuel Ndashyikirwa ya kusimamia mauaji ya mamia ya watu katika eneo la Kibongo nchini Rwanda.

Hata hivyo katika kesi hiyo ndugu hao wawili walishikilia kwamba hawakuhusika katika mauaji hayo.

Wawili hao wanaishi Ubelgiji ambapo wameshatakiwa.

Umoja wa Mataifa unakisia idadi ya watu wapatao laki nane waliuwawa katika mauaji ya halaiki nchini Rwanda.