1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Biashara ya nguo kujadiliwa.

26 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhi

Maafisa wa umoja wa Ulaya na wale wa China wameanza mazungumzo yao mjini Beijing yenye lengo la kupitia upya mkataba wa kibiashara ambao umesababisha bidhaa kadha za nguo kutoka China kuzuiwa na maafisa wa forodha wa umoja huo.

Makubaliano hayo ya kibiashara ambayo yalifikiwa mwezi wa Juni yamekuja kutokana na kuingia kwa wingi kwa nguo za bei rahisi kutoka China zinazoingia katika umoja wa Ulaya , kufuatia kuondolewa kwa viwango vya uingizaji nguo duniani. Lakini viwango vipya kuhusiana na uingizaji wa nguo kutoka China tayari vimekwisha fikiwa.

Hii imesababisha idadi kadha ya nguo kulundikana katika bandari za Ulaya na mabohari.