1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Blinken alaani uchokozi wa Korea Kaskazini

Angela Mdungu
14 Julai 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekan Anton Blinken, vitendo vya Korea kaskazini kurusha makombora na matumizi ya silaha za maangamizi. Ni katika mkutano wa Jumuiya ya kusini mashariki mwa Asia, ASEAN

https://p.dw.com/p/4TvUQ
ASEAN-Außenministertreffen in Jakarta
Picha: Dita Alangkara/Pool/REUTERS

Katika majadiliano yaliyohusisha wanadiplomasia wa zaidi ya mataifa 24 waliokutana Indonesia, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Antony Blinken ametoa wito kwa mataifa yanayounda Jumuiya ya Indo-Pasific kuwa kitu kimoja ili kukomesha matumizi ya silaha za maangamizi pamoja na kurusha makombora.

Ametaka pia kuwepo kwa utulivu katika kanda hiyo  na kwamba hakuna changamoto kubwa kwa usalama wa kanda hiyo zaidi ya uchokozi wa kurusha makombora unaofanywa na Korea kaskazini.

Soma zaidi:Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Blinken ahimiza utulivu katika Indo-Pasifiki

Lavrov akasirishwa na ukosoaji

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amekasirishwa na ukosoaji dhidi ya uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell Picha: Jean-Francois Badias/AP/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya Jumuiya ya kanda ya , Mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema Lavrov alimjibu kwa ukali kuwa kila kitu kinachoendelea kinatokana na nadharia za kufikirika za magharibi na kwamba vita vitaendelea kwani Urusi haiko tayari kuachana na vita na kuondoa majeshi yake Ukraine.

Tukisalia katika mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Indonesia Retno Marsudi amesema kuwa, mkutano wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia umekubaliana kuimarisha diplomasia ya kujilinda. Marsudi ametambua pia ongezeko la mivutano inayoendelea kuigawanya kanda hiyo na kwamba changamoto hiyo inazidi kuwa kubwa. Ukanda huo unapambana kuutatua mzozo wa Myanmar ambayo utawala wake unashutumiwa vikali kwa ukatili dhidi ya raia.