1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Blinken ahimiza utulivu kanda ya Indo-Pasifiki

14 Julai 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa utulivu katika kanda ya Indo-Pasifiki na kuuhimiza ulimwengu kushirikiana ili kuikomesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4TthU
Indonesien Südostasien Wang Yi und Antony Blinken
Picha: Dita Alangkara/AP Photo/picture alliance

Kauli hiyo aliitoa baada ya mkutano wa pande mbili na mwenzake wa Indonesia Retno Marsudi mjini Jakarta ambako alihudhuria mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia - ASEAN

Aidha, Blinken ametoa wito wa kile alichokielezea kuwa ni amani ya kudumu kwa vita vya uchokozi vya Urusi nchini Ukraine na kuwahimiza watawala wa kijeshi wa Myanmar kusitisha uhasama na kuanzisha mazungumzo.

Blinken pia alifanya mazungumzo na mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi, ikiwa ni sehemu ya kile Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema ni msururu wa mikutano inayolenga kuweka wazi njia za mawasiliano.