1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akutana na Mfalme Charles III na waziri mkuu Sunak

10 Julai 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amekutana na Mfalme Charles III wa Uingereza wakati wa ziara fupi ya siku moja mjini London kabla ya kuelekea Lithuani kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4Tgfe
Windsor | Rais Biden akutana na Mfalme Charles
Rais Joe Biden wa Marekani na Mfalme Charles III wa UingerezaPicha: Andrew Matthews/Getty Images

Rais Joe Biden wa Marekani amekutana na Mfalme Charles III wa Uingereza wakati waziara fupi ya siku moja mjini London kabla ya kuelekea Lithuani kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Biden alimtembelea Mfalme Charles kwenye kasri la Windsor kwa mazungumzo yaliyotuama juu ya masuala ya mazingira, moja ya ajenda za kipaumble za mfalme huyo wa Uingereza.

Hapo kabla Biden alikuwa na mkutano na waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak katika ofisi zake za mtaa wa Downingambapo walikubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirika baina ya nchi zao mbili na pamoja na kuendelea kuiunga mkono Ukraine.

Sunak na Biden wamekutana mara kadhaa katika kipindi cha miezi michache iliyopita katika wakati kiongozi huyo wa Uigereza anajaribu kurekebisha mahusiano yake na Washington yaliyotiwa doa a kipindi cha msukosuko wa utawala Boris Johnson na Liz Truss.