1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kukutana na Waziri Mkuu Sunak Jumapili

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kuwasili Uingereza leo kwa ziara fupi itakayomkutanisha na Waziri Mkuu Rishi Sunak na kujadili masuala ya mazingira na Mfalme Charles kuelekea mkutano wa NATO.

https://p.dw.com/p/4TdPT
Marekani Washington
Rais Joe Biden wa Marekani Picha: Samuel Corum/abaca/picture alliance

Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kuwasili Uingereza leo kwa ziara fupi itakayomkutanisha na Waziri Mkuu Rishi Sunak na kujadili masuala ya mazingira na Mfalme Charles kuelekea mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami NATO.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani ya White House imesema ziara hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili. Biden atakutana na Sunak ikiwa ni mwezi mmoja baada ya viongozi hao wawili kukubaliana mjini Washington juu ya Azimio la Atlantiki na ushirikiano zaidi katika masuala ya teknolojia, nishati safi na madini.

Mazungumzo yao huenda yakajumuisha mkutano ujao wa kilele wa NATO na vita vya Ukraine. Baada ya mazungumzo, viongozi hao wataelekea nchini Lithuania kushiriki mkutano wa kilele wa NATO.