1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Zawadi ya euro 50,000 ya kukamatwa mtuhumiwa

24 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIh

Serikali nchini Ujerumani imesema Walebanon wawili waliokuwa wakishukiwa kutega mabomu kwenye treni za abiria nchini Ujerumani yumkini kabisa kwanza walikimbilia Lebanon baada ya njama yao kushindwa.

Akizungumza kwenye televisheni ya Ujerumani mkuu wa polisi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Joerg Ziercke amesema mmojawapo wa watuhumuwa ambaye hivi sasa yuko mbaroni alikuwa amerudi kutoka Lebanon.Mtu huyo mwenye umri wa miaka 21 anayetambulika kwa jina la Youssef Mohamed alikamatwa na polisi katika mji wa kaskazini wa Kiel hapo Jumamosi.

Mtuhumiwa wa pili ambaye polisi inasema ni Mlebanon mwenye umri wa miaka 20 anayeitwa Jihad Hamad bado yuko mitini.

Serikali ya Ujerumani inatowa zawadi ya euro 50,000 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa Hamad.