1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Dunia yalaani mauaji ya mbunge Lebanon

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOC

Viongozi mbalimbali duniani pamoja na wanasiasa nchini Lebanon wamelaani shambulizi la bomu lililomuua mbunge maarufu wa Lebanon ambaye ni mpizani wa Syria.

Antoine Ghanem aliuawa pamoja na watu wengine wanane katika kitongoji kinachokaliwa na wakristo wengi nje kidogo ya mji mkuu wa Beiruti.

Jumuiya ya kimataifa imelaani mauaji hayo ikisema yana nia ya kuvuruga uchaguzi mkuu wa rais nchini Lebanon uliyopangwa kufanyika wiki ijayo.

Mauaji ya mbunge huyo ni ya hivi karibuni dhidi ya watu maarufu wanaoipinga Syria na alikuwa miongoni mwa wanachama w anane wa kundi wanaopinga udhibiti wa Syria nchini humo, toka kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Harir mwaka 2005