1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Mapigano katika kambi ya wakimbizi yamemalizika.

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpa

Waziri wa ulinzi wa Lebanon amesema kuwa wapiganaji wa Kiislamu waliojificha katika kambi ya wakimbizi ya Wapalestina karibu na mji wa kaskazini wa Tripoli wameshindwa na kwamba operesheni iliyochukua muda wa mwezi mzima ya kijeshi imemalizika.

Elias Murr amesema katika mahojiano katika televisheni kuwa jeshi hivi sasa linajihusisha na operesheni ya usafi na kwamba kambi hiyo itabakia imezimezingirwa hadi pale wapiganaji waliobaki wa kundi la Fatah al-Islam watakapojisalimisha.

Wakimbizi wa Kipalestina maelfu kadha wanasemekana kuwa bado wako ndani ya kambi hiyo.