BEIRUT: Lebanon kufanya mageuzi ya kiuchumi
3 Januari 2007Matangazo
Libnan inajiandaa kuanzisha mageuzi ya kiuchumi ikiwa na lengo la kuwavutia wafadhili. Waziri mkuu wa Libnan, Fouad Siniora jana alizindua mpango huo, unaojumulisha ubinafsishaji unaonuiwa kuongeza uwekezaji na kupunguza deni la taifa.
Hatua hiyo inafanyika siku chache kabla mkutano wa wafadhili uliopangwa kufanyika baadaye mwezi huu mjini Paris, Ufaransa. Mpango wa mageuzi ya kiuchumi utawasilishwa katika mkutano huo.
Waziri Siniora anasema deni la Libnan limeongezeka na kufikia dola bilioni 40 za kimarekani, huku kiasi cha takriban dola bilioni tano cha deni hilo, kikiwa kimesababishwa na vita baina ya Israel na wanamgambo wa kundi la Hezbollah.