1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kujitoa kwenye mkataba unaokataza majaribio ya nyuklia

25 Oktoba 2023

Baraza la juu la bunge la Urusi limeidhinisha sheria inayolenga kuiondoa Urusi kwenye mkataba wa kimataifa wa kupiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia.

https://p.dw.com/p/4Y0QA
Bunge la Urusi likiwa katika vikao vyake
Bunge la Urusi likiwa katika vikao vyakePicha: Sergei Fadeichev/dpa/TASS/picture alliance

Hiyo ni hatua ya mwisho kabla ya sheria hiyo kupelekwa kwa Rais Vladimir Putin kwa ajili ya kutia saini.

Baraza la Shirikisholiliidhinisha sheria hiyo kwa pamoja bila pingamizi kwa kura 156.

Soma pia:Urusi kwenye hatua za mwisho kujiondowa Mkataba wa Nyuklia

Mapema mwezi huu, Rais Putin aliwahimiza wabunge kufanya mabadiliko ili kuakisi msimamo wa Marekani ambayo ilitia saini mkataba huo lakini haikuidhinisha kikamilifumkataba wa marufuku dhidi ya majaribio ya silaha za nyuklia.

Urusi inasema haitarejelea majaribio ya nyuklia endapo Marekani nayo haitafanya.