1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi wa Urusi akagua kombora la kisasa

7 Oktoba 2023

Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amekagua kiwanda cha silaha za kijeshi kinachotengeneza kombora la masafa marefu aina ya Sarmat. Kombora hilo ni kati ya makombora ya kutumainiwa ya kizazi kijacho ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4XFC2
Jaribio la kombora la Samarat yaliyofanyika Urusi mwaka 2022
Jaribio la kurusha kombora la Samarat yaliyofanyika Urusi mwaka 2022Picha: Russian Defence Ministry/AFP

Waziri Shoigu amesema kombora hilo la masafa marefu litakuwa ni msingi wa kambi ya ndani ya vikosi vya kimkakati vya nyuklia vya Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, siku ya Alhamis alisema kwamba Urusiinakamilisha matengenezo ya kombora hilo, ambalo litaimarisha uwezo wa kijeshi wa vikosi vyake na kuhakikisha usalama wa Urusi dhidi ya vitisho kutoka nje.

Serikali ya Kremlin ambayo inakabiliwa na vikwazo kutoka mataifa ya Magharibi, imeongeza matumizi katika sekta ya ulinzi kwa asilimia 68 kwa mwaka ujao wa 2024.