1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ukraine yaushambilia mji wa Urusi kwa ndege zisizo na rubani

Sylvia Mwehozi
1 Septemba 2023

Ukraine imefanya shambulio la ndege isiyo na rubani katika mji wa magharibi mwa Urusi ambao una moja ya kinu kikubwa cha nishati ya nyuklia nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Vpki
Russland | Baustelle Atomkraftwerk Kursk II
Picha: Tatyana Simonenkova/TASS/IMAGO

Gavana wa mji wa Kursk Oblast Roman Starovoit amesema kuwa shambulio hilo, limeharibu sehemu ya mbele ya jengo katika mji wa Kurchatov, kilometa chache kutoka kinu cha nyuklia cha Kursk mapema leo Ijumaa.

Kinu hicho cha nishati ya nyuklia cha enzi ya Dola ya Kisovieti kinatumia kwa pamoja makaa na urani kufua nishati sawa na kinu cha nyuklia cha Chernobyl. Mlipuko na moto uliotokea katika kinu cha Chernobyl mwaka 1986, ulikuwa ni ajali mbaya zaidi duniani iliyoeneza mionzi ya nyuklia kote Ulaya.

Mamlaka za Urusi pia zimedai kuitungua droni nyingine karibu na Moscow   mapema leo na kutatiza kwa muda safari za ndege.