1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa Tigray walibaka, kupora na kuwapiga wanawake

10 Novemba 2021

Shirika la Human Rights Watch limesema mzingiro wa serikali ya Ethiopia dhidi ya mkoa wa Tigray unawazuwia wahanga wa ubakaji uliofanywa na pande hasimu katika mzozo uliodumu mwaka mzima sasa, kupata huduma za afya.

https://p.dw.com/p/42oP1
Tigray-Konflikt I TPLF-Kämpfer
Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images

Ripoti ya Human Rights Watch imetokea wakati mmoja na ripoti ya shirika la Amnesty International ambayo imesema waasi wa Tigray, walibaka, kupora na kuwapiga wanawake wakati wa shambulio kwenye mji mmoja mkoani Amhara.

Human Rights Watch imezituhumu pande zinazopambana kwa kutenda uhalifu mkubwa wa kingono na kuvilenga kwa makusudi vituo vya afya, ikiorodhesha madhila ya kimwili na kiakili yanayowakumba wahanga wa ubakaji wenye umri wa hadi miaka 80.

Ripoti hiyo imesema wahanga wa ubakaji walihitaji matibabu ya magonjwa ya zinaa, mifupa iliyovunjika, majeraha ya kuchomwa visu na msongo wa mawazo.

Soma pia: TPLF yapuuza ripoti kwamba inapingwa mjini Addis Ababa

Siyo tu wanawake na wasichana wa Tigray wamekabiliwa na ukiukaji wa kutisha, ripoti hiyo imesema pia wanakabiliwa na ubahaba wa chakula, dawa na msaada mwingine unaohitajika kujenga upya maisha yao.

Äthiopien | Treffen Getachew Reda, Olusegun Obasanjo und Debretsion Gebremichael
Mjumbe wa Umoja wa Afrika Olusegun Obasanjo akiwa katika mkutano na viongozi wa kundi la TPLF Getachew Reda na Debretsion Gebremichael, wakati alipofanya ziara mkoani Tigray Novemba 7, 2021.Picha: Privat

Uchunguzi wa Amnesty Internatiional, ambao ulitokana na mahojiano na manusura 16 wa mashambulizi ya kingono katika mji wa Nifas Mewcha, ulifuatia tipoti ya awali ya shirika hilo la haki za binadamu iliyoainisha ubakaji wa mamia ya wanawaje na wasichana uliofanywa na wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea mkoani Tigray.

Ripoti ya Jumatano imejikita kwenye mashambulizi ya mwezi Agosti ya kundi la Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, ambapo wanawake 14 kati ya 16 waliohojiwa waliielezea Amnesty kwamba walibakwa kimakundi na waasi, katika baadhi ya visa kwenye mtutu wa bunduki na wakati watoto wao wakiangalia.

Katika moja ya matukio yaliofafanuliwa na Amnesty, Gebeyanesh, ambaye siyo jina lake halisi, alisema wapiganaji wa TPLF walimbaka wakiwa katika kundi, huku watoto wake wenye umri wa miaka tisa na kumi wakilia.

Soma pia:Makundi 9 yaunda muungano kumpinga Abiy 

Mama huyo mwenye miaka 30, alisema walipiga makofi na mateke huku wakiweka bunduki zao kama vile wanakwenda kumfyatulia risasi.

Wengi wa wabakaji hao walikuwa wanatumia maneno ya kashfa ya kikabila, ambapo mama mmoja wa watoto wawili aliiambia Amnesty kwamba mmoja wa wanaume wanne waliomshambulia alimuita punda wakati binti yake akiona.

Ätopien | Unterstützer des Premierministers feiern
Raia wakiwa wamebeba bango lenye picha ya waziri mkuu Abiy Ahmed wakati wa maandamano ya kuiunga serikali na kulaani kile waandaji walisema ni kundi la TPLF, katika uwanja wa Meskel mjini Addis Ababa, Ethiopia, Novemba 7, 2021.Picha: Tiksa Negeri/REUTERS

Kamatakamata dhidi ya Watigray?

Vita hivyo vinavyoendelea tangu Novemba 2020, vimekumbwa na matukio ya mauaji ya kikatili na ubakaji wa watu wengi, huku maelfu ya watu wakiuawa na milioni mbili wakipoteza makazi yao.

UN ilisema pia Jumatano kwamba Ethiopia iliwakamata maderea 72 wanaolifanyia kazi shirika la programu ya chakula duniani katika mji wa kaskazini kwenye barabara pekee inayofanya kazi kuelekea mkoa wa Tigray.

Soma pia: Ethiopia yatangaza hali ya hatari nchi nzima

"Tunaweza kuthibisha kwamba madereva 72 waliopewa kandarasi na WFP wamekamatwa mjini Semera. Tunawasiliana na serikali ya Ethiopia kufahamu sababu za kukamatwa kwao," alisema msemaji wa UN.

Habari za kukamatwa kwa madereva hao zimejiri siku moja baada ya UN kusema wafanyakazi wake 22 raia wa Ethiopia wamekamatwa katika mji mkuu Addis Ababa kufuatia uvamizi ambao mawakili na mashirika ya haki za binadamu yanasema ulilenga watu wa kabila la Tigray.

Chama cha TPLF chawakabili wanajeshi wa Ethiopia Tigray

Sita kati ya wafanyakazi hao waliachiwa wakati waliobakia 16 walikuwa kizuwizini Jumanne usiku, msemaji wa UN Stephan Dujjarric aliwaambia waandishi habari kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York.

Soma pia:Marekani yasema TPLF kuilenga Addis Ababa ni kitisho kikubwa 

Tume iliyoteuliwa na serikali ya haki za binamu ilisema Jumapili kwamba ilipokea ripoti nyingi kuhusu kukamatwa kwa Watigray katika mji mkuu, wkiwemo wazee na kina mama wenye watoto.

Polisi hata hivyo ilikanusha kuendesha msako wenye mwelekeo wa kikabila, wakisema kwamba wanawalenga waungaji mkono wa vikosi vya waasi wa Tigray vinavyopigana dhidi ya serikali kuu.

Chanzo: Mashirika