1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TPLF yapuuza ripoti kwamba inapingwa mjini Addis Ababa

8 Novemba 2021

Wapiganaji wa mkoa wa Tigray wanaopambana na serikali kuu ya Ethiopia wamepuuza ripoti kwamba watakabiliwa na raia wenye ghadhabu au kusababisha umwagikaji damu ikiwa watasonga mbele kuingia mji mkuu, Addis Ababa.

https://p.dw.com/p/42iN6
Ätopien | Unterstützer des Premierministers feiern
Picha: Tiksa Negeri/REUTERS

Hayo yanajiri mnamo wakati siku ya Jumapili maelfu ya watu waliandama katika mji mkuu wakiunga mkono jeshi. 

Siku ya Jumapili, maelfu ya raia waliandamana katika mji mkuu Addis Ababa kuunga mkono serikali ya Abiy Ahmed na jeshi la shirikisho linalopambana na vikosi vya Tigray na washirika.

Baadhi ya waandamanaji waliikashifu Marekani, ambayo ni moja kati ya nchi ambazo zimetaka mapigano hayo ambayo yamechacha katika wiki za hivi karibuni kusitishwa.

Soma: Marekani yasema TPLF kuilenga Addis Ababa ni kitisho kikubwa

Soma: Makundi 9 yaunda muungano kumpinga Abiy

Hata hivyo, katika wiki za hivi karibuni, kundi la wapiganaji wa TPLF limedai kupata ushindi huku likikamata miji iliyoko umbali wa kilomita 400 kutoka mji mkuu Addis Ababa.

Msemaji wa TPLF Getachew Reda amesema ripoti kwamba raia katika mji mkuu wa Addis Ababa wanawapinga ni suala ambalo limeongezewa chumvi na kichekesho.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019, alipeleka wanajeshi wake katika jimbo la Tigray Novemba 2019, kupambana na vikosi vya TPLF.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019, alipeleka wanajeshi wake katika jimbo la Tigray Novemba 2019, kupambana na vikosi vya TPLF.Picha: Office of the Prime Minister Ethiopia/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Japo wanamgambo hao wanaweza kulenga mji wa Addis ili kulikamata kuwawezesha kumpindua serikali ya Abiy, anasema hilo si lengo lao maalum.

"Kwetu sisi, lengo letu kuu si Addis Ababa. Hatuna haja haswa na Addis Ababa. Lengo letu ni kuhakikisha Abiy hawi kitisho kwa watu wetu tena,” amesema Reda.

Reda ameongeza pia kwamba chama cha TPLF ambacho kilitawala siasa za Ethiopia kwa takriban miaka 30 hadi Abiy alipochukua mamlaka mwaka 2018, hakina haja ya kuchukua madaraka ya taifa hilo

Nchi kadhaa zimewatahadharisha raia wao kuondoka Ethiopia. Tayari Marekani ilishawaondoa wanadiplomasia wao wakati machafuko hayo yaliyoanzia mkoa wa kaskazini yakishamiri.     

Wapiganaji kutoka mkoa wa Tigray Tigray People's Liberation Front (TPLF) pamoja na washirika wao wamekuwa wakipigana na serikali kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
Wapiganaji kutoka mkoa wa Tigray Tigray People's Liberation Front (TPLF) pamoja na washirika wao wamekuwa wakipigana na serikali kwa muda wa mwaka mmoja sasa.Picha: picture alliance/AA

Umoja wa Mataifa, Baraza lake la Usalama, Umoja wa Afrika, Kenya na Uganda zimetoa miito ya kutaka usitishaji vita hivyo ambavyo vimewaua maelfu ya watu katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Canada ambayo imetaja hali nchini Ethiopia kuwa inayobadilika na inazidi kudorora kwa haraka, imeshawaondoa maafisa wake wa ubalozi wake ulioko nchini humo pamoja na familia zao.

Siku ya Ijumaa iliyopita, serikali ya Abiy iliahidi kuendelea kupambana ikisema ina wajibu wa kuilinda nchi. Serikali hiyo ilizitaka nchi za nje kusimama na Ethiopia.

Maelfu ya watu tayari wameuawa kufuatia makabiliano hayo na wengine wameachwa katika mazingira magumu katika taifa hilo kubwa lililoko mashariki mwa Afrika.

Ethiopia yatangaza hali ya hatari

Mnamo Novemba mwaka uliopita, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019, alipeleka wanajeshi wake katika jimbo la Tigray baada ya kuwashutumu wapiganaji wa jimbo hilo kwa kushambulia kambi za jeshi la serikali ya shirikisho.

Tume Haki za binadamu ya Ethiopia ambayo makamishna wake huteuliwa na serikali, ilisema siku ya Jumapili kwamba inaonekana maafisa wanatumia sheria ya hali ya hatari iliyotangazwa Jumanne wiki iliyopita kuwa sababu ya kuwakamata watu kwa misingi ya makabila yao.

(AFPE, RTRE)