1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo kati ya Israel na Hezbollah wazusha wasiwasi mkubwa

24 Juni 2024

Afisa mkuu wa jeshi la Marekani ameonya kwamba shambulio lolote la kijeshi la Israel nchini Lebanon litasababisha shambulio la kulipiza kisasi la kundi lenye nguvu la wanamgambo wa Hezbollah wanaofadhiliwa na Iran.

https://p.dw.com/p/4hPnd
Lebanon - Kiongozi wa kundi la Hezbollah, Hassan Nasrallah
Kiongozi wa kundi la Hezbollah la huko Lebanon, Hassan NasrallahPicha: EPA/WAEL HAMZEH

Jenerali wa Jeshi la Anga CQ Brown amesema makabiliano hayo yanaweza kupelekea kutanuka kwa vita na hivyo kuviweka vikosi vya Marekani katika hatari eneo hilo.

Soma pia: Mivutano ya Israel-Hezbollah yaongeza hofu ya kutanuka vita vya Gaza

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hapo jana kuwa anatumai kufikiwa kwa suluhisho la kidiplomasia lakini akasisitiza kuwa na uwezo wa kutatua tatizo hilo kwa njia tofauti ikiwa itahitajika.

Waziri wa Ulinzi wa Israel  Yoav Gallant  anatarajiwa kujadili suala zima la mzozo wa Mashariki ya Kati katika ziara yake iliyoanza jana nchini Marekani.