1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant aelekea Marekani

23 Juni 2024

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant leo hii aelekea Washington kwa mazungumzo "muhimu" kuhusu vita vya Gaza vilivyoanza tangu Oktoba 7 na kuzidisha mvutano wakutishia kuvuka mpaka kwa kulijumuisha kundi la Hezbollah.

https://p.dw.com/p/4hPIy
Waziri wa Ulinzi wa Israel Joav Gallant
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant anatembelea wanajeshi katika eneo la Rafah. Picha: Ariel Hermoni/Israel Mod/IMAGO

Awali Gallant amesema "atajadili maendeleo huko Gaza na Lebanon, na kuapa kwamba wako tayari kwa hatua yoyote ambayo inaweza kuhitajika huko Gaza, Lebanon na katika maeneo ya ziada.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alielezea matumaini ya maendeleo ya haraka katika kuruhusu tena utoaji wa silaha kutoka kwa Marekani, mshirika mkuu wa Israel ambao alisema umeshuka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni. Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akitofautiana na kiongozi huyo mkongwe wa mrengo wa kulia wa Israel kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vifo vya raia Gaza.