1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel-Hezbollah waongeza hofu ya kutanuka vita vya Gaza

20 Juni 2024

Hofu juu ya vita imeongezeka baada ya Kundi la Hezbollah kusema kwamba hakuna sehemu ya Israel itakayokuwa salama, ikiwa vita kamili vitazuka.

https://p.dw.com/p/4hJti
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah
Mivutano kati ya Israel na Hezbollah inaongeza hofu ya kutanuka vita vya GazaPicha: EPA/WAEL HAMZEH

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema hakuna sehemu ya Israel itakayonusurika na makombora ya Hezbollah, ikiwa vita vitazuka.

Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran, limekuwa linashambuliana na Israel kila siku tangu wapiganaji wa Hamas walipoishambulia kusini ya Israel tarahe 7 Oktoba.

Soma pia: Hezbollah yaendeleza mashambulizi ya kisasi dhidi ya Israel

Mashambulizi ya ndege za Israel, roketi za Hezbollah na matumizi ya silaha nyingine yameongezeka katika uhasama baina ya pande mbili hizo mnamo wiki za hivi karibuni. Kiongozi wa Hezbollah pia ameitishia Cyprus ikiwa itairuhusu Israel itumie viwanja vyake vya ndege kuishambulia Lebanon.