1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la uchaguzi laendelea DR Kongo

20 Desemba 2023

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inafanya uchaguzi mkuu ambapo Rais Felix Tshisekedi anawania muhula wa pili madarakani dhidi ya upinzani uliogawika na chini ya kiwingu cha ukosefu wa usalama mashariki mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4aP13
DR Kongo | Uchaguzi wa rais 2023
Uchaguzi wa rais DR Kongo 2023Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Uchaguzi unaendeleakwenye maeneo mengi ya taifa hilo, licha ya  hapo kugubikwa na ucheleweshaji wa kufunguliwa vituo vya kupigia kura ikiwemo kwenye mji mkuu, Kinshasa.

Zaidi ya wapiga kura milioni 44 wamesajiliwa kushiriki uchaguzi wa leo wa rais, bunge la taifa, mabunge ya mikoa na madiwani.

Soma pia: Wakongomani wapiga kura leo kuchagua viongozi wapya

Rais Tshisekedi aliyeingia madarakani mwaka 2019 anawania muhula mwingine wa miaka mitano akichuana na wagombea wengine 18. Anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena, licha ya upinzani kutoka kwa wanasiasa wengine ikiwemo mfanyabiashara maarufu Moise Katumbi.