Zelensky awahimiza viongozi wa EU kuridhia uanachama wake
14 Desemba 2023Matangazo
Akihutubia mkutano huo kwa njia ya video, Zelensky amewaomba viongozi hao kutowasaliti watu na imani yao kwa Ulaya.
Zelenskyameongeza kuwa leo ni siku muhimu na kwamba iwapo itakuwa njema ama mbaya kwa nchi hiyo, matukio yake yataingia katika historia.
Soma pia:Zelensky ahimiza nchi wanachama wa EU na Marekani kuipa Ukraine misaada zaidi ya kifedha
Miongoni mwa viongozi wa mataifa 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, ni waziri mkuu wa Hungary pekee Viktor Orban aliyepinga kuanzishwa kwa mazungumzo hayo na Ukraine wakati taifa hilo linapoendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
Kwakuwa maamuzi kama hayo yanahitaji kuungwa mkono na mataifa yote wanachama, Umoja wa Ulaya hauwezi kuruhusu kujumuishwa kwa Ukraine bila kuidhinishwa na Orban.