1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky anatarajiwa kukutana na Biden mjini Washington

12 Desemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden atampokea rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwenye Ikulu ya Marekani hii leo katika juhudi za kulishinikiza bunge lake kusitisha mkwamo wa kuidhinisha usaidizi zaidi wa kijeshi kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4a4Aq
Diplomasia | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Biden amemualika Zelensky mjini Washington kusistiza msimamo wa Marekani aliosema hautatetereka katika kuwaunga mkono watu wa Ukraine wakati wanapojilinda na uvamizi kutoka Urusi. 

Taarifa kutoka Ikulu inasema viongozi hao wawili watajadiliana juu ya mahitaji muhimu ya Ukraine na umuhimu wa Marekani kuendelea kuiunga mkono katika wakati huu mgumu. 

Soma pia:Bunge la Marekani lagawika kuhusiana na msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine

Zelensky anapanga kukutana na wanachama bunge la Congress akiwemo spike wa bunge wa chama cha Republican Mike Johnson. Hii ni ziara ya tatu ya Zelensky tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini humo February 24 mwaka jana.

Kifungu kingine cha msaada mpya kwa Ukraineumezuwiwa kufuatia mivutano ya ndani ya kisiasa kati ya wademokrats na warepublican. Wanachama wa Republican wamekuwa na mashaka juu ya kuendelea kuinga mkono Ukraine.