1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ataka raia wa Ukraine wapambane kuilinda nchi

22 Desemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atoa wito kwa wananchi wenzake kuendelea kuwa na moyo wa mapambano kwa ajili ya ulinzi wa nchi yao, ikiwa ni siku chache tu kabla ya sherehe za Krismasi.

https://p.dw.com/p/4aSwm
Volodymyr Zelensky
Picha: AFP/Getty Images

Katika ujumbe wake wa jana usiku, Zelensky amesema sasa ni wakati wa kuisaidia Ukraine kutimiza malengo yake, akiongeza kuwa muda wa kupumzika utakuja baadae. Rais huyo wa Ukraine amesema hatima ya nchi itaamuliwa katika maeneo ya Kharkiv, Luhansk, Donestk, Zaporizhzhya na Kherson, ambayo yameshambuliwa na Urusi.Hayo ni wakati ndege za Urusi zisizoruka na rubani zilishambulia mji mkuu Kyiv na miji mingine ya Ukraine jana usiku. Kulingana na taarifa za awali kutoka kwa utawala wa kijeshi wa Kiev, vipande vya ndege isiyo na rubani vilianguka kwenye jengo la makazi lililoko kusini-magharibi mwa jiji.