1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky apongeza juhudi za kurejesha umeme

13 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanaokarabati miundombinu ya nishati iliyoharibiwa na mashambulizi ya Urusi Ijumaa iliyopita, wanafanya kazi nzuri.

https://p.dw.com/p/4NPGY
Ukraine Kiew | Wolodymyr Selesnkyj
Picha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Zelenskiy amesema watu hawajakabiliwa kwa kiasi kikubwa na hali ya ukatikaji umeme. Hata hivyo ametahadharisha kwamba ni mapema sana kutangaza ushindi katika vita vinavyolenga miundombinu ya nishati.

Hayo yakijiri, vikosi vya Ukraine vinalinda ngome zao katika uwanja wa mapambano mashariki mwa Donetsk, ikiwemo mji unaoshambuliwa wa Bakhmut, huku mapigano makali ya kukamata miji ya Vuhledar, na Maryinka yakiendelea.

Katika tukio jingine, katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya  NATO Jens Stoltenberg , atakamilisha muhula wake wa kuiongoza jumuiya hiyo mwezi Oktoba.

Msemaji wa NATO Oana Lungescu amesema madaraka ya Katibu Mkuu Jens Stoltenberg yameshaongezwa mara tatu na amehudumu kwa takriban miaka tisa.