1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu Mkuu wa NATO apanga kuondoka madarakani mwezi Oktoba

12 Februari 2023

Jumuiya ya Kujihami ya NATO imefahamisha leo kuwa, kiongozi wake wa muda mrefu Jens Stoltenberg hana mpango wa kuongeza muda wake wa uongozi kwa mara ya nne na anatarajia kuachia nafasi hiyo mwezi Oktoba.

https://p.dw.com/p/4NODp
Norwegen Oslo | NATO Generalsekretät Jens Stoltenberg
Picha: Terje Bendiksby/NTB/picture alliance

Msemaji wa NATO, Oana Lungescu amesema madaraka ya Katibu Mkuu Jens Stoltenberg yameongezwa mara tatu na amehudumu kwa takriban miaka tisa.

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Norway mwenye umri wa miaka 63 alichukua wadhifa huo katika makao makuu ya NATO  mjini Brussels Oktoba 1, 2014 na ameusimamia muungano huo wa Magharibi kupitia migogoro kadhaa ya kimataifa.

Wanadiplomasia kutoka washirika kadhaa wa NATO  walikisia kwamba muda wa Stoltenberg unaweza kuongezwa kwa mara nyingine hadi mkutano wa kilele mwaka ujao wa kuadhimisha miaka 75 ya muungano huo.