1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky aomba msaada zaidi wa ulinzi wa anga

30 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelalamika kuhusu mashambulizi yanayoendelea ya Urusi na kwa mara nyingine tena ameomba msaada zaidi wa ulinzi kutoka nchi za Magharibi.

https://p.dw.com/p/4hh3p
Rai wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aomba msaada zaidi kutoka kwa washirika wake.Picha: Ukraine Presidency via Bestimage/IMAGO

Zelensky amesema katika kipindi cha wiki moja, Urusi imefyetua mabomu 800 kuelekea Ukraine, huku akichapisha video za uharibifu mkubwa katika maeneo ya Kherson, Dnipro, Odessa na Zaporizhzhya.

Akisisitiza hoja yake, rais Zelensky amesema Ukraine inahitaji mifumo zaidi ya ulinzi wa anga, msaada zaidi kutoka kwa washirika wake na inahitaji mbinu ya kushambulia na kukabiliana na wapiganaji wa Urusi.

Soma pia: Biden aapa kuimarisha msaada kwa Ukraine

Nchi za Magharibi zinaiunga mkono Ukraine katika kampeni yake ya kujihami dhidi ya Uvamizi wa Urusi, ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka miwili.