1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky alihutubia bunge la Ujerumani

17 Machi 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelihutubia Bunge la Ujerumani la Bundestag na kusema Urusi inajenga "ukuta"  ndani ya bara la Ulaya kwa kuishambulia nchi yake huku akiomba msaada zaidi kutoka Berlin.

https://p.dw.com/p/48d1P
Deutschland Bundestag | Rede Wolodymyr Selenskyj
Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Wakati uvamizi wa Urusi ukiendelea, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amezungumza na wabunge wa Ujerumani kwa njia ya video na kuwaomba msaada zaidi. Mzozo huo umekuwa ukisababisha pia kauli na mivutano ya kidiplomasia. Bakari Ubena ana ripoti zaidi.

Zelensky alisema ukuta huo una "nguvu zaidi" na unawazuia raia wengine wa bara la Ulaya kuona mateso yaliyopo nchini Ukraine. Ameitaka Ujerumani kuunga mkono jitihada ya Ukraine ya kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Soma pia:Baraza la Ulaya Laitimua Urusi

Zelensky pia aliikosoa Ujerumani kwa kuchelewesha kufutwa kwa Nord Stream 2, ambao ni mradi wenye utata wa bomba la gesi asilia linalotoka Urusi hadi Ujerumani.

Alisema rufaa nyingi za Ukraine zilizohimiza kuachana na mradi huo kutokana na uvamizi wa Urusi, ziligonga mwamba kutokana na matarajio ya kiuchumi.

China yaweka neno kwenye mzozo huo

China inayotazamiwa kuwa mpatanishi katika mzozo huu inapinga vikali kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ya kwamba msimamo wa China kutolaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine hauendani na msimamo wa nchi hiyo kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Singapur | Rüstungsgeschäft mit Taiwan | Zhao Lijian
Zhao Lijian msemaji wizara ya mambo ya nje ChinaPicha: Imago Images

Zhao Lijian msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China alisema kauli kama hizo hazisaidii na kuyataja matramshi hayo ni kashfa dhidi ya China ambayo inafichua kikamilifu fikra za Marekani ya vita baridi.

"Matamshi kama haya hayasaidii kutatua tatizo, na China inayapinga vikali." Alisema Zhao na kuongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken aliishutumu taifa hilo kuwa katika upande mbaya wa historia.

Ukraine:Putin atambulike kama mhalifu wa kivita

Jana Jumatano, Waziri wa ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov aliwaambia wabunge wa Umoja wa Ulaya kuwa wanapaswa kumtambua Rais wa Urusi Vladimir Putin kama mhalifu wa kivita baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Indien | Friedensprotest in Bhopal
sanaa katika kuhimiza kusimamishwa mapigano UkrainePicha: Sanjeev Gupta/SOPA Images/ZUMA/picture alliance

Alitoa mfano wa shambulio la anga la Urusi kwenye jumba la maonyesho siku ya Jumatano ambapo alisema wanawake 1,200 na watoto walikuwa wamejificha kuyakimbia mashambulizi ya vikosi vya Urusi.

Kauli kama hiyo ilitolewa pia j na Rais wa Marekani Joe Biden alimuita  Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa ni mhalifu wa kivita.

Ikulu ya Kremlin ilisema kauli hiyo haisameheki huku Urusi ikikanusha kuwalenga raia na kusisitiza kuwa haikushambulia ukumbi wa michezo.

Soma pia:Urusi na Ukraine zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku nzima

Dakika moja ya ukimya imeshuhudiwa katika vituo vya treni nchi Ukraine vikiwemo vya Dnipro, Lviv, Odessa na Kyiv ili kutoa heshima kwa wahanga wa mashambulizi katika uvamizi unaondelea wa Urusi nchini Ukraine.

Katika utaratibu wake wa kawaida wa kutoa taarifa kwa njia ya video Rais Zelensky alisema, amewaambia raia wake wote kuwa na utaratibu wa  kila waianzapo siku kutumia walau dakika tatu kuwakumbuka wote walioathirika na mbashambulizi ya vikosi vya Urusi ikiwemo waliofariki, tangu kuanza kwa mashambulizi mnamo Februari 24 majira ya asubuhi.