1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelenskiy: Tuko tayari kufanya uchaguzi tukipata ufadhili

28 Agosti 2023

Rais wa Ukraine, akijibu wito wa seneta wa Marekani aliyetaka atangaze kufanyika uchaguzi mwaka 2024, amesema uchaguzi utafanyika wakati vita vikiendelea iwapo washirika wao wa Magharibi watatoa ufadhili.

https://p.dw.com/p/4VdGc
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: kyodo/dpa/picture alliance

Katika mahojiano na shirika la habari la 1+1, Zelenskiy amesema amejadiliana juu ya suala hilo la kuandaa uchaguzi na seneta Graham ikiwemo ufadhili na uhitaji wa kubadilisha sheria ya wakati wa kuandaa uchaguzi.

Wabunge kadhaa wa Marekani walifanya ziara mjini Kyiv Agosti 23, miongoni mwao seneta Lindsey Graham, aliyeisifu Ukraine kwa mapambano yake dhidi ya Urusi japo ameeleza umuhimu wa nchi hiyo kufanya uchaguzi.

Katika mazingira ya sasa, uchaguzi hauwezi kufanyika nchini Ukraine chini ya sheria ya kijeshi, ambayo lazima iongezwe muda kila baada ya siku 90 na sheria ya sasa inatarajiwa kukamilika Novemba 15, baada ya tarehe ya kawaida ya Oktoba ambamo hufanyika kura za ubunge japo kabla ya uchaguzi wa urais ambao ungefaa kufanyika mnamo mwezi Machi mwaka 2024.